Jules Mugiraneza: Shida ya kuzama kwenye ziwa Kivu inapita kipimo
Hali ya usafiri kwenye Ziwa Kivu inaleta tatizo kubwa, ambalo lilisababisha ajali mbaya iliyotokea tarehe tatu Oktoba karibu na bandari ya Kituku huko Goma. Baada ya kuzungumza na walionusurika na familia za wahasiriwa, mwanabunge wa kitaifa mchaguliwa wa Masisi, Jules Mugiraneza anataja upakiaji wa kupitisha kiasi, hali mbaya ya boti